BY ISAYA BURUGU,21ST MARCH,2023-Kenya imeungana na ulimwengu hivi leo kuadhimisha siku ya upandaji miiti duniani wito ukitolewa kwa wakaazi wa Narok kupanda miti kwa wingi ili kupiga jeki juhudi za serikali kuafikia miti bilioni 15.

Naibu gavana wa kaunti ya Narok Tamalinye Koech vilevile amesema juhudi hizo zitapelekea kuimarisha utunzaji mazingira nchini Koech akizungumza katika shule ya kibinafsi ya Ongata mjini Narok wakati alipongoza zoezi la upanzi wa miti ,ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti ya Narok kupanda miti manyumbani, shuleni na maeneo mbali hasa katika ardhi ya umma.

Pia  ameshabikia ushirikiano uliopo miogoni mwa Wenyeji wa kaunti hii katika upandaji  miti. Naibu gavana amesema kuna maeneo ambayo yamesalia kama ardhi tambarere hatua ambayo imepelekea maeneo mbali mbali kaunti ya Narok kukosa mvua kwa muda mrefu.

 

 

 

 

 

March 21, 2023