Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati amefariki akiwa na umri wa miaka 63. Chebukati alifariki katika hospitali ya Nairobi kufuatia kuugua kwa muda mrefu.

Wakili kitaaluma, Chebukati aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa IEBC na aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta mnamo Januari 2017 huku muhula wake wa miaka sita ukikamilika Januari 17, 2023. Alichukua wadhifa huo kutoka kwa Ahmed Issack Hassan.

Rais William Ruto amemuomboleza aliyekuwa Chebukati kama kiongozi mwenye kanuni na bidii aliyetumikia taifa kwa uadilifu. Ruto alitaja kifo cha Chebukati kuwa pigo kubwa kwa nchi.

February 21, 2025

Leave a Comment