BY ISAYA BURUGU,13TH MARCH,2023-Aliyekuwa Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi  hatashatakiwa mahakani  kuhusiana  na uchapishaji waujumbe juu ya uvamizi wa boma lake na polisi mtaani Karen mnamo tarehe 8 mwezi jana.

Hii ni baada ya  mkurugenzi mkuu wa mashataka ya umma Noordin Haji kusema kuwa Ushahidi uliyowasilishwa  na idara ya upelelezi wa jinai DCI  dhidi ya Matiangi na wakili wake Danstan Omari hautoshi kuwafungulia wawili hao mashataka

.Kwenye taarifa Haji ameiagiza DCI kufunga faili juu ya swala hilo na kusitisha hatua yoyote ya polisi.DCI ilikuwa imewasilisha faili ya kesi hiyo kwa DPP kufanya ukaguzi na kutoa mapendekezo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

March 13, 2023