BY ISAYA BURUGU,13TH MARCH,2023-Aliyekuwa makamu wa rais wat isa nchini Moody Awori amewataka wanasiasa kuachana na vita vya ubabe wa kivita na kuunga mkono utawala war ais William Ruto ili uweze kutekeleza manifesto yake.Akizungumza baada ya mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi kumtembelea nyumbani kwake jijini Nairobi, Awori mwenye umri wa miaka 94 amesema wanasiasa wanapasw akuwa katika mstari wa mbele kuwaunganisha wakenya.
Matamshi yake yanakuja wakati kinara wa upinzani Raila Odinga anafanya mikutano yakitaifa kuwaraia wafausi wake kukatalia mbali utawala wa Ruto.Odinga aliyepoteza kwa Ruto katika uchaguzi mkuu wa Agosti mwaka jana, anasisitiza kuwa zoezi hilo lilibiwa na amekuwa akiuta utawala wa Ruto kama usiokuwa halali.
Kwa mjibu wa Awori Ruto anahitaji heshima , na ungwaji mkono kutoka kwa kila mkenya anapoongoiza nchi.