BY ISAYA BURUGU,14TH MARCH,2023-Katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala amefichua vyama ambavyo tayari vimeamua kujiunga na UDA kuwa chama kimoja.Akizungumza na wandishi Habari,Malala amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa rais Wiliam Ruto anakuwa na wakati bora anapoongoza taiafa kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao.

Vyama vilivyoamua kujiunga na UDA ni Pamoja na Chama Cha Kazi (CCK), kinachohuishwa na Waziri wa biashara na viwanda Moses Kuria na chama cha  Chama Cha Mashinani (CCM) kinachongozwa na  Isaac Ruto.

Vingine ni Umoja na Maendeleo kinachongozwa naye aliyekuwa gavana wa  Embu  Martin Wambora, National Agenda Party of Kenya ,Farmers Party (Irungu Nyakera) na Economic Freedom Party ( Issack Hassan Abey).

Malala amewasihi viongozi wa vyama hivyo kuwakaribisha wannachama wao ndani ya mwavuli wa UDA ili kujenga chama hicho.

 

 

 

 

March 14, 2023