BY ISAYA BURUGU,15TH MARCH,2023-Meneja wa kituo cha huduma katika kaunti ya Narok Everlyne Katampoi amewataka wananchi wote ambao walituma maombi ya kupata vitambulisho kufika kituo hicho kuvichukuwa.

Akiongea katika kituo hicho mjini Narok Bi. Katampoi amesema kwamba kufikia sasa tangu mwaka uliopita kuna zaidi ya vitambulisho 2700 ambavyo vingali kuchukuliwa na wenyewe.

Meneja huyo ametoa changamoto kwa wakaazi ambao bado hawajachukuwa stakabadhi hizo kuchukuwa hatua ya kuchukuwa ili kupunguza mrundiko unaoshuhudiwa kwa sasa katika kituo hicho cha huduma.

Kando na vitambulisho vile vile Bi. Katampoi ameongeza kwamba kuna mirundiko ya vyeti vya kuzaliwa ambavyo pia havijachukuliwa.Kufikia sasa anasema kuna vyeti vya kuzaliwa elfu moja na hapo kusisitiza haja ya wazazi kufika pale na kuchukuwa.

 

 

 

March 15, 2023