BY ISAYA BURUGU,18TH MARCH,2023-Mwanamme wa miaka  39  ambaye ni baba wawatoto wanne  anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Njoro kaunti ya Nakuru baada ya kukamatwa akijaribu  kumsaidia bintiye wa miaka 18 kuavya mimba.

Mwaname huyo anadaiwa kuwa ndiye aliyempachika bintiye mimba yenyewe.Naibu chifu wa lokesheni ndogo ya Amani Milka  Langat amesema mwanamme huyo alikuwa amekwenda kumchukua bintiye kutoka shuleni Kitale katika kaunti ya Tras Nzoia  akiwa na lengo la kutekeleza uovu huo.

Msichana huyo anasemekana kuwa na ujauzito wa miezi mitatu.Mwanamme huyo anasemekana kuhadaiwa  na  wanavijiji  kusafiri hadi nyumbani  kutoa mimba ya bintiye kabla ya kupelekwa hadi maeneo ya vichochoro mjini Njoro.

Langat amesema msichan ahuyo alikiri  kulazimishwa kushiriki ngono na babake  kwa miaka minne  na kusema kuwa alipojaribu kumhusisha mamake  alionywa kuwa angeliona cha mtema kuni.Mwanamme huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya polisi kukamilisha uchunguzi.

 

 

 

 

March 18, 2023