BY ISAYA BURUGU,20TH MARCH,2023-Usalama umeimarishwa katika sehemu mbali mbali nje na ndani ya jijini kuu Nairobi siku ambayo mungano wa Azimio la umoja umepanga kufanya mandamano.Uchunguzi uliyofanywa na Redio Osotua umebaini kuwa katika sehemu ambazo kwa kawaida ulinzi hua ni mkali katika siku za kawaida.Usalama umeimarishwa mara dufu.

Sehemu hizo ni Pamoja na ikulu ya Nairobi ambapo usalama umeongezwa kwenye barabara za kuelekea na kutoka katika ikulu hiyo ,afisi ya rais iliyoko jumba la harambee katika barabara ya harambee,afisi na majengo ya serikali iliyoko karibu ikiwemo bunge la kitaifa na lile la seneti kati ya  maeneo mengine.

Mungano wa Azimio ulitangaza mandamano kote nchini huku uongozi wa mungano huo ukishinikiza serikali kupunguza gharama ya kimaisha.Usalama pia umeimarishwa kwenye miji mingine mikuu ya Nakuru,Mombasa na Kisumu.

 

 

 

 

 

 

 

 

March 20, 2023