BY ISAYA BURUGU,20TH MARCH,2023-Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi  na seneta  wa Kilifi  Stewart Madzayo  wamekamatwa jijini Nairobi katika mandamano ya Azimio yanayoendelea.

Mandamano hayo yameandaliwa kupinga kupanda kwa gharama ya Maisha.Taarifa zasema kuwa wawili hao  walikamatwa katika jumba la mikutano la KICC  ambapo walikuwa wamejiunga na  wandamanaji  wengine akiwema seneta Edwin Sifuna.Idadi isiyojulikana ya wandamaji pia wamekamatwa   katika maeneo mbali mbali jijini  huku polisi wakijizatiti kuzima mandamano hayo.

Maafisa wa polisi walilazimika   kufyatua vitao machozi kuwatawanya wandamanaji hao.Mandamano makubwa na makabiliano yameshuhudiwa eneo la kibra ambapo wakaazi wameonekana wakiwarushia polisi mawe  huku polisi wakijibu kwa kurusha vitao machozi.Wakati haya yakifanyika barabara zote za kuelekea ikulu zimesalia kuwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.

 

 

 

 

 

RIPOTI YA UN

March 20, 2023