Gavana wa kaunti ya Kisumu Prof. Anyang’ Nyong’o amelaani vitendo vya uharibifu wa mali vilivyoshuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya kaUnti hiyo, kufuatia maandamano yaliyoandaliwa ili kulalamikia ongezeko la gharama ya Maisha.
Kupitia taarifa aliyochapisha jioni ya leo, Gavana Nyong’o ameeleza kusikitishwa na uharibifu wa mali ulioshuhudiwa katika baadhi ya maduka, hoteli, benki n ahata dukakuu katika kaunti hiyo.
Gavana Nyong’o ameeleza kwamba wahalifu waliojiunga na waandamanaji walivamia wafanyabiashara na kuwasabishia hasara hiyo, jambo ambalo amelikashifu na kuzitaka asasi za usalama kuanzisha uchunguzi ili kuwanasa wahusika.
Ofisi za chama cha UDA eneo la Nyalenda katika kaunti hiyo pia zilivamiwa, huku gari moja lililokuwa limeegeshwa likiteketezwa.
PRESS STATEMENT ON HOOLIGANISM DURING KISUMU DEMONSTRATIONS. pic.twitter.com/J68C8TvgXK
— Gov. Anyang' Nyong'o (@AnyangNyongo) March 20, 2023