BY ISAYA BURUGU,21ST MARCH,2023-Viongozi wa Kenya Kwanza wamekashfu  mandamano ya hiyo jana yaliyoandaliwa na mungano wa Azimio la umoja .Katika kikao na wandishi habari viongozi hao wakiongozwa na gavana wa Embu Cicil MBarire wanasema kuwa mandamano hayo yaliyipelekea Kenya kupoteza mamilioni ya pesa huku wananchi wakawaiada wakihangaika kutokana na shughuli zao za kiuchumi kuadhirika.

Sasa wanaitaka idara ya polisi kufanya uchunguzi kuhusu mandamano hayo na kuhakikisha kuwa wahusika wananchukuliwa hatua za kisheria.

Vilevile wanamtaka msajili wa vyama vya kisiasa kusitisha mgao wa fedha unaoelekezwa katika chama cha ODM baada ya afisi za chama cha UDA kuvamiwa na kuteketezwa moto  na wandamanaji jana ili fedha hizo zigaramie hasara iliyotokea.

.Azimio imetangaza kuwa itakuwa inandaa mandaano kama hayo kila jumatatu.

 

March 21, 2023