BY ISAYA BURUGU,22ND MARCH,2023-Hali ya hofu na majonzi imekumba kijiiji cha Nyamakoroto kata ndogo ya sungututa eneo bunge la kitutu Masaba kaunti ya Nyamira baada ya mtu na mkewe kupatikana wameuawa ndani ya nyumba yao.

Edward Morema mwenye umri wa miaka 63 ambaye ni mkaazi wa marekani na mkewe Grace Morema wa miaka 60 walipata jana alasiri wakiwa na majeraha ya visu kichwani na mwilini huku wakiwa wamefungwa mikono na miguu kwa nyaya.

Naibu kamanda wa polisi wa Masaba kaszikazini Robert Ndambiri  amedhibitisha kisa hicho na kusema kuwa uchunguzi umeanzishwa huku wafanyikazi wawili wa boma hilo wakitiwa mbaroni.

March 22, 2023