Rais William Ruto amekashifu maandamano ya Raila Odinga dhidi ya serikali yaliyopangwa kufanyika Jumatatu na Alhamisi kila wiki.

Katika maoni mafupi ya kuchekesha Mkuu wa Nchi ameonyesha matumaini kwamba siku hizo mbili hivi karibuni zitakuwa siku ambazo zitarekodi idadi kubwa zaidi ya biashara katika Soko la Hisa la Nairobi.

Aidha Ruto ameapa kukabiliana na watu binafsi wanaolenga kuzuia maendeleo ya kiuchumi ya taifa.Rais Ruto amekariri kujitolea kwake kukuza uchumi wa taifa, maono ambayo atayalinda vikali ili yatimizwe.

March 22, 2023