Tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu KHRC, imelaani hatua ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwadhibiti Wananchi waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga serikali yaliyoandaliwa na muungano wa upinzani siku ya Jumatatu.

Katika taarifa yake, tume hiyo imeeleza kwamba asasi za usalama zilitumia nguvu kupita kiasi katika baadhi ya maeneo kulikoandaliwa maandamano, badala ya kuwapa ulinzi wanapotekeleza maandamano hayo abayo yamekubalika kikatiba.

Aidha polisi pia wameshtumiwa kwa kuinglia shughuli za waandishi wa habari na kuwazuia baadhi ya wanahabari waliokuwa wakiangazia matukio kwenye maandamano yao kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

KHRC imeitaka IPOA Pamoja na idara ya huduma za polisi kuchunguza na kuwashtaki waliohusika katika vitendo hivi.

March 29, 2023