Watu 14 wamethibitishwa kufariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani katika barabara kuu ya Nakuru-Naivasha iliyohusisha basi la Chuo Kikuu cha Pwani na matatu ya abiria.

Kulingana na ripoti, basi hilo lilikuwa likiwasafirisha takriban watu 30, miongoni mwao wanafunzi na walimu, kuelekea mashindano ya michezo ajali hiyo ilipotokea leo adhuhuri.

Watu kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali za karibu kwa matibabu ya haraka.

Baadhi ya viongozi wa kisiasa akiwemo spika wa bunge la seneti Amason Kingi wametoa rambirambi zao kwa familia ambazo zmewapoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo.

March 30, 2023