BY ISAYA BURUGU 31ST MARCH,2023-Mwili wa Jeff Mwathi umefukuliwa katika zoezi lililoendeshwa na maafisa wa idara ya uhalifu wa jinai.Mwili huo ulifukuliwa kwa ajili ya uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo chake. Uchunguzi utafanywa kisha baadaye mwili wake utazikwa tena.

Mkurugenzi wa DCI Amin Mohammed alitoa tangazo hilo alipoandamana na wachunguzi hadi Redwood Apartments ambapo Jeff Mwathi alifariki baada ya kuanguka kutoka kwenye jengo hilo. Hatua hiyo inakuja baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa DNA na Toxicology.Amin  na maafisa wake wanatathmini  upya eneo la uhalifu ambapo Jeff aliripotiwa kufariki akiwa nyumbani kwa msanii maarufu wa Kikuyu DJ Fatxo.

Mohamed anataka uchunguzi wa tukio hilo ufanywe haraka ili kubaini kama kulikuwa na mchezo usio wa kawaida katika kifo cha Mwathi.

Mnamo Februari 22, mwathiriwa alidaiwa kuanguka kutoka kwenye dirisha la ghorofa ya 10 la jumba la Redwood kwake DJ Fatxo, jina halisi Lawrence Njuguna alipokuwa akiburudika  na marafiki zake.

 

 

March 31, 2023