Rais William Ruto amesema wanafunzi 20,000 wa vyuo vikuu watanufaika na mafunzo ya ziada baada ya shule yaani internship kuanzia mwaka ujao.

Amesema kuna haja ya kuwapa wanafunzi zaidi fursa ya kutumikia nchi kupitia mpango huo.

Rais amezitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha vijana wengi zaidi wananufaika na mpango huo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuinua maisha yao.

Rais alisema hayo  wakati wa uzinduzi wa mpango wa mafunzo ya utumishi wa umma  katika jumba la Kimataifa la Mikutano KICC, Nairobi.

Wanafunzi 3,902 walinufaika na mpango huo mwaka huu.

Hali kadhalika Dkt Ruto alipongeza Tume ya Utumishi wa Umma kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi walioajiriwa wanaakisi sura ya Kenya.

March 31, 2023