BY ISAYA BURUGU,5TH APRIL,2023-Mtu mmoja ameripotiwa kufariki huku wanafunzi kadhaa wakijeruhiwa baada ya basi mbili za shule kugongana ana kwa ana kwenye barabara ya Kagio kuelekea Baricho kaunti ya Kirinyaga leo asubuhi.Wakaazi waliokuwa karibu walikimbia kwenye eneo la tukio kujaribu kuwaokoa manusura kwenye magari hayo mawili huku maafisa wa polisi wakiwasili kutathmini hali.

Kulingana na picha zilizopigwa wakati wa mkasa huo ,magari hayo mawili yaligongana kwa upande,huku madirisha na baadhi ya sehemu za mbele zikiharibiwa.Mwili wa mtu aliyefariki umepelekwa katika hifadhi ya maiti  katika hospitali ya Kerugoya.

Kwa mjibu wa polisi ni kwamba  meneja wa shule ya Trinity Academy amelazwa katika hospitali ya  Kagio nursing home akiwa na majeraha mabaya huku wanafunzi  wanane waliojeuhiwa wakipelekwa katika hospitali  ya Kerugayo.

 

 

April 5, 2023