BY ISAYA BURUGU,6TH APRIL,2023-Uongozi wa shirika la michezo lililobuniwa na kampuni za maji hivi leo umemtembelea gavana wa Narok Patrick Ntuntu afisini mwake kumjuza kuhusu juhudi zake za ustawshaji michezo katika kaunti hii.

Ukiongozwa na Peter Kamau,uongozi huo umesema kaunti ya Narok iko katika mkondo unaofaa kupiga jeki maswala ya michezo na kumshukuru gavana kwa msaada wake katika kufanikisha azimio hilo.Kwa upande wake gavana Ntutu amesema utawala wake utaendelea kutoa msaada wowote hitajika kadri ya uwezo wake kustawisha maswala ya michezo katika kaunti hii.

Haya yanajiri huku matayarisho kuelekea katika uzinduzi wa awamu ya 12 ya michezo chini ya shirika hilo yakayozinduliwa na kuandaliwa katika kaunti hii ya Narok mwezi Agosti mwaka huu yakiendelea.

Baadaye gavana ameongoza hafla ya upandaji miti katika juhudi za kukabili adhari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye kaunti hii.Gavana amendamana na naibu gavana Tamalinye Koech na kamishna wa kaunti hii Isaac Nasinde kati ya wengine.

 

 

 

April 6, 2023