Chama cha Muungano wa Azimio la Umoja kimetangaza kikosi cha Viongozi saba wanaotarajiwa kuwakilisha mrengo huo katika mazungumzo ya kutafuta mwafaka katika shughuli ya uteuzi wa makamamishena wa tume ya IEBC.

Chama hicho kinachoongozwa na Raila Odinga kimetaja orodha hiyo, kama mojawapo ya matakwa waliyopendekeza kuelekea kwa mazungumzo hayo yaliyotangazwa na Rais William Ruto. Viongozi waliotajwa katika orodha hiyo ni:

  1. Seneta wa Narok Ledama Ole Kina
  2. Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna
  3. Seneta wa Kitui Enoch wambua
  4. Mbunge wa Malindi Amina Mnyanzi
  5. Mbunge wa Mbita Millie odhiambo
  6. Mbunge wa Pokot Kusini David Kosing
  7. Mbunge wa Rarieda Otiende Amolo

Muungano huo ulipendekeza kamati maalum itakayoendesha mazungumzo hayo nje ya bunge, jambo ambalo limepingwa vikali na muungano wa Kenya kwanza.

Kinara wa Muungano huo aidha alitangaza kwamba mpango wa kuandaa maandamano ungali hai iwapo mikakati ya mazungumzo haya haitazaa matunda yoyote.

April 6, 2023