BY ISAYA BURUGU ,10TH APRIL,2023-Chama cha ODM kimepuzilia mbali  taarifa kuwa kimewabadilisha viongozi wa chama hicho katika kaunti ya Kakamega.Kupitia taarifa  iliyotolewa leo,Chama hicho  kimedai kuwa kimepokea taarifa  zinazodai kuwa  kumekuwa na mageuzi ya uongozi wa  chama katika kaunti hiyo.

ODM ikizitaja ripoti hizo  kama zakupotosha ,a kusema kuwa  hakuna uchaguzi  ua mabadiliko ya viongozi yatakayofanywa  bila bodi yakitaifa ya chama hicho kutoa idhini kama inavyohitajika kisheria.

Wameweka bayana kuwa mabadiliko katika uongozi wa chama   ni sharti yapitie katika uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa baadaye mwaka huu .

Chama hicho kimesema kuwa walio na nia ya kujiuzulu ni sharti wafuate utaratibu uliyoko.Wakati huo huo  walio na nia ya kuwania nafasi mbali mbali chamani huo wameshauriwa  kuanza kujifahamisha na kanuni zinazosimamia uchaguzi wa mashinani  kusubiri tarehe ya uchaguzi wenywe.

 

 

April 10, 2023