Rais William Ruto anatarajiwa kuongoza shughuli ya utoaji wa Ripoti ya kutadhmini Utendakazi wa wizara mbalimbali, mashirika ya Serikali Pamoja na Taasisi za elimu ya juu ya mwaka uliopita wa kifedha wa 2021/22 hapo kesho, katika hafla itakayoandaliwa kwenye ukumbi wa KICC jijini Nairobi.

Kutolewa kwa ripoti hii, ni mojawapo ya njia za serikali kufuatilia utendakazi wa idara na wizara mbalimbali, ili kuhakikisha kwamba kazi zinazohitajika zinatekelezwa ipasavyo. Katika agizo la rais lililochapishwa mwezi Januari mwaka huu, Rais alitangaza kuwa mkuu wa mawaziri nchini atakuwa na jukumu la kuangazia utendakazi wa wizara na mashirika ya serikali.

Viongozi mbalimbali kutoka serikali ya kitaifa na zile za kaunti Pamoja na wawakilishi wa sekta za kibinafsi wanatarajiwa kuhudhuria hafla yenyewe.

April 10, 2023