BY ISAYA BURUGU,11TH APRIL,2023-Washukiwa watatu wanaoshutumiwa kuhusika na kifo cha mhubiri wa eneo la Mt Elgon wamekamatwa.Idara ya upelelezi wa jinai DCI, inasema washukiwa hao wamewekwa kwenye rumande kwa kuhusika na kifo cha David Ngeiwa ambaye aliuawa kinyama  tarehe 7, Machi 2023 katika eneo la Kaptama, Mt Elgon kaunti ya Bungoma.

Visa vingi vya utovu wa usalama vimeripotiwa katika eneo hilo la Mlima Elgon huku viongozi wa eneo hilo wakimtaka Inspekta Jenerali wa polisi, Japheth Koome kuchukua hatua mwafaka ili kudhibiti usalama wa wananchi wa eneo hilo dhidi ya makundi ya majambazi.

Aidha mbunge wa Kimilili Didmus Barasa pia alisema kuwa uhamisho wa maafisa wa eneo hilo unafaa kufanywa kwa kuwa wamekua kwa kituo moja cha polisi kwa muda wa miaka 15.

 

 

April 11, 2023