BY ISAYA BURUGU,15TH APRIL,2023-Makachero  kutoka eneo la Starehe wamewakamata washukiwa wawili wanaohusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha Utalii mwenye umri wa miaka 25.Job Chihonyi aliuawa yapata kilomita chache kutoka chuo anuai cha Utalii katika barabara ya Thika tarehe 5 mwezi Feburuari mwaka huu.

Washukiwa hao    Kevin Ngechu  na Maxwell Omukuba wanasemekana kumvamia  Chihonyi, kumuiabia simu yake kabla ya kumdunga kwa kisu kifuani na kumuacha amefariki kabla ya kutoroka kutumia pikipiki.

Idara ya upepelezi wa jinai kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter  imesema simu ya mkononi inayoaminika kupatikana kwa njia za uhalifu ilipatikana  kwa Kevin Ngechu  huku pikipiki nyeusi yenye nambari za usajili KMGF 828K  iliyotumiwa kama njia ya kutorokea katika siku ya tukio pia ilipatikana.

Washukiwa hao wawili wamo mikoni mwa polisi na wanatarajiwa kushatakiwa kwa kosa la mauaji.

April 15, 2023