Serikali ya kitaifa na ile ya Kaunti ya Narok zitashirikiana ili kuimarisha miradi ya ujenzi wa mabwawa na kuhakikisha upatikanaji wa maji ya matumizi kwa wakaazi wa kaunti hii. Haya ni kwa mujibu wa Rais William Ruto, ambaye alieleza kwamba serikali hizi mbili zimetenga kima cha shilingi milioni 300 kwa miradi yam aji katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Narok.

Akizungumza mapema leo katika eneo la Limanet viungani mwa mji wa Narok alikozindua mradi wa usafishaji wa majitaka, Rais alieleza kuwa serkali haitakoma katika juhudi zake za kuhakikisha kwamba kila mkenya anapata maji safi na salama ya matumizi.

Aidha rais amewasifia wakulima katika kaunti ya Narok kwa juhudi zao za kuzalisha chakula, akieleza kwamba wakulima wamejitokeza kwa idadi za juu ili kununua mbolea na mbegu ili kuhakikisha kwamba tatizo la ukame linakabiliwa ipasavyo. Rais aliandamana na viongozi wengine wakiwemo wale wa kaunti hii wakiongozwa na gavana Patric Ntutu.

Kwa upande wake gavana wa Narok amemwomba rais kupiga jeki miradi inayoendelea ya ujenzi wa mabwawa, huku akieleza kwamba wananchi wa kaunti hii hawako tayar kujihusisha katika shughuli za maandamano.

YouTube player

 

April 15, 2023