Waziri wa elimu nchini Ezekiel Machogu ametangaza mabadiliko katika usimamizi wa shule ya upili ya Mukumu huku akimhamisha mwalimu mkuu wa shule hiyo Frida Ndolo pamoja na kuivunja Bodi ya Usimamizi, baada ya wanafunzi watatu na mwalimu mmoja kuaga dunia kutokana na ugonjwa unaodaiwa kusababishwa na ulaji wa chakula kilichoathirika.
Waziri huyo aliyezuru shule hiyo kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa taarifa za mkurupuko wa maradhi hayo, amepongeza juhudi zilizowekwa na idara za afya ili kuhakikisha kwamba maradhi hayo hayaenei Zaidi.
Shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa katika kipindi cha majuma 2 yajayo, Waziri wa elimu akieleza kwamba serikali itafuta gharama yote ya matibabu ya wanafunzi walioathirika.