BY ISAYA BURUGU,18TH APRIL,2023-Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Wanguru  kule mwea mashariki kauntiti ya Kirinyaga  wamemtia mbaroni mwanamme anayeshukiwa kumbaka btinye wa umri wa miaka miwili unusu.

Mtoto huyo  anaripotiwa kuachwa na mamake aliyekuwa ametofautiana na babake  wakati kisa hicho kilipotokea.Wakaazi wa Kijiji cha Kaimbu waliitikia kilio cha mtoto huyo  lakini mwanamme huyo alitoroka.kisha baadaye akakamatwa muda mfupi baadaye.

Akidhibitisha kisa hicho OCPD wa Mwea mashariki James Mutua amesema polisi walijibu baada ya kilio kutoka kutoka kwa wananchi.

April 18, 2023