BY ISAYA BURUGU,18TH APRIL,2023-Takriban wanafunzi 6 wamefariki kufuatia ajali mbaya ya barabarani eneo la Delamare Naivasha kaunti ya Nakuru.

Wanafunzi hao walikuwa wakisafiri kutoka Magharibi mwa Kenya kuelekea Nairobi ajali ilipotokea.

Sita hao walikufa papo hapo.

Ajali hiyo ilihusisha lori na matatu iliyokuwa imewabeba wanafunzi hao.

Wengine 10 waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali ya kaunti ya Naivasha kwa matibabu.

April 18, 2023