Azimio maandamano

BY ISAYA BURUGU,19TH APRIL,2023-Kikoa  cha mungano   wa Azimio  la umoja kilichonua kuandaliwa kaunti ya Muranga hiyo kesho kimefutiliwa mbali.Kamanda wa polisi wa Muranga David Mathiu amekatalia mbali ombi la Azimio kuandaa mkutano huo  akisema maafoisa wa polisi wamepewa jukumu kwingineko  na walihitaji kuarifiwa mapema ili kufanya mandalizi.

Kwa mjibu wa Mathiu ,ilani ya mkutano  inapaswa kuwa ingetumwa siku nne kabla na Azimio waliwasilisha ombi hilo siku mbili kabla ya mkutano huo.

Hivyo basi mkutano huo hautaruhusiwa.Mkutano huo ulinuiwa kuhudhuriwa na viongozi wanaoegemea murngo wa Azimio wakiwemo  Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, Martha Karua, George Wajackoyah and Mwangi wa Iria na  Jeremiah Kioni.

Aliyekuwa gavana wa Muranga alikuwa katika kituo cha polisi cha Muranga hiyo jana kuwasilisha notisihiyo akisema mkutano huo utakuwa na lengo la  kutoa fursa kwa viongozi hao kuzungumza na wenyeji ili kusaka jisni ya kuhusishwa ndani ya serikali.

 

 

 

April 19, 2023