BY ISAYA BURUGU,19TH APRIL,2023-Viongozi katika bunge la kaunti ya Kilifi wametishia kushiriki mandamano kushinikiza kuchukuliwa kwa hatua kali kwa mhubiri tata Paul Makenzi anayezuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi Pamoja na wafuasi wake.

Viongozi hao wakiongozwa na spika wa bunge hilo Teddy Mwambire wanasema kuwa mhibiri huyo sharti achunguzwe na akipatikana na hatia afunguliwe mashataka.

Aidha wanasema kuwa hawatakubali wakaazi wa Kilifi washikilie Imani potovu ya kanisa hilo  la Makenzi ambalo limechangia ambayo imechangia maafa kwa baadhi ya wafausi waliolazimishwa kufunga.Mahama iliamuru mhubiri huyo azuiliwe kwa siku 14 ili kuwaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi wao

.

 

 

 

 

 

April 19, 2023