Rais William Ruto amemteua aliyekuwa Gavana wa Meru Kiraitu Murungi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Kitaifa la Mafuta.

Kulingana na Notisi ya Gazeti la tarehe 20 Aprili 2023, Kiraitu atashikilia wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu.

Pia aliyekabidhiwa wadhfa katika awamu ya hivi punde ya uteuzi ni aliyekuwa Gavana wa Tharaka Nithi Samuel Ragwa ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao na aliyekuwa Naibu Gavana wa Makueni Adelina Mwau kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa jumba la Kimataifa la Mikutano KICC.

Mkuu wa Nchi pia amemteua aliyekuwa mgombea Urais David Mwaure Waihiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa hazina ya kitaifa ya Mazingira kwa kipindi cha miaka mitatu.

April 21, 2023