BY ISAYA BURUGU,22ND APRIL,2023-Mwanamme wa miaka 25 anauguza majeraha baada ya kuvamiwa na umati uliojawa na hasira kwa  kumua mwanamke wa miaka 22 kuhusiana na mzozo wa kimapezni mjini Kitengela kaunti ya Kajiado.Marehemu anaripotiwa kukataa ombi la mwanamme kutaka kuwa naye kwenye mahusiano hatua iliyompelekea mwanamme huyo kumdunga kisu.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kajiado Muthuri Mwongera amedhibitisha kisha hicho cha usiku wa kuamkia leo  kilichotokea katika hoteli moja akisema mshukiwa ambaye ni mwenzake marehemu  katika hoteli hiyo aliondoka kazini mapema  kabla ya kurejea tena na kumsubiri mwanamke huyo nje na kutekeleza kitendo hicho.

Walioshuhudia kisha walimvamia mwanamme huyo na kumwacha na majeraha mabaya.Mwongera amesema mshukiwa kwa sasa anaendelea kupokea matibabu  katika hospitali moja huko Kitengela chini ya ulinzni mkali akisubiri kufikishwa mahakamani siku ya jumatatu.Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya Shalom uchunguzi ukiendelea.

 

 

April 22, 2023