BY ISAYA BURUGU 25TH APRIL,2023-Mwanamke wa miaka 27  katika mtaa wa  Milimani  kule kitengela  kaunti ya Kajiado amemdunga kisu na kumua mtoto wake wa umri  wa miaka miwili  na baadaye kula mwili wa mtoto huyo

.Majirani wamesema  kuwa  Olivia Naserian alijifungia   ndani ya nyumba na alikuwa akicheza na mtoto kabla ya kugeuka na kuzua fujo huku akiharibu vyombo vya nyumba .Kelele  kutoka kwa vyombo vilivyokuwa vikivunjwa iliwavutia majirani  waliofika na kushuhudia Naserian akimdunga kisu mtoto huyo kwa jina Gloria Njeri mara kadhaa kwani hawangeweza kuingia katika nyumba hiyo iliyokuwa imefungwa.

Majirani waliwapasha polisi Habari  walioweza kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba na kumpata mshukiwa akiwa amepoteza fahamu.Akidhibitisha kisa hicho OCS wa Kitengela David Shani amesema kuwa mwanamke huyo alimkata mtoto huyo vipande vipande  na kula matumbo yake Pamoja na figo.

Mwanamke huyo alipelekwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kitengela kwa matibabu  na kulazimishwa kutabika vipande hivyo vya mwili ambavyo vitatumiwa kama Ushahidi.Majirani wanadai kuwa mwanamke huyo alimuua mwanawe baada ya kudaiwa kuachana na mumewe.

 

 

April 25, 2023