BY ISAYA BURUGU 25TH APRIL,2023-Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amefika kule Shokahola ambapo opareseni ya uopoaji wa miili inaendelea.Pia mikakati inaendelea sambamba kuwaokoa wale ambao bado wako hai.Tayari miili 73 imefukuliwa katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Hiyo jana msaidizi mkuu wa mhubiri Paul Mackenzie aliyefahamika kama pastor Zablon  alikamatwa na pia yeye anazuiliwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani.

Pia jana miii 26 ilipolewa huku shughuli hiyo ikirejelewa leo.Miili kumi Zaidi imepatikana leo mitano ilipatikana katika kaburi la Pamoja.

Watu wawili pia wamepatikana wakiwa hai wote wakiwa ni wanawake.Kabla ya kufika eneo la tukio huko shakahola,Waziri Kindiki kwanza ameandaa mkutano wa faragha na kamishna wa  kaunti ya Kilifi  na maafisa wengine.

 

 

 

 

April 25, 2023