Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amependekeza kushtakiwa kwa Kasisi Bandia Paul Makenzi na makosa ya Mauaji ya halaiki, kufuatia vifo vilivyoshuhudiwa katika eneo la Shakahola katika kaunti ya Kilifi.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo bada ya kuzuru eneo hilo ambalo limeshuhudia miili zaidi ya 89 ikifukuliwa katika makaburi yanayoaminika kuandaliwa na waumini wa Imani iliyokuwa ikifunzwa na Makenzi, alisema kando na shtaka la kigaidi linalopendekezwa na mkurugenzi wa mashtaka ya jinai nchini, Makenzi anafaa kushtakiwa kwa kosa la mauaji ya halaiki kwa mujibu wa sheria za Kenya na pia za Kimataifa.
Kindiki pia alitangaza kwamba shamba la Ekari 800 linaloaminika kumilikwa na Makenzi ni eneo litakalowekwa chini ya ulinzi wa serikali ili kuendeleza operesheni ya uokozi na pia ufukuzi
Waziri huyo aidha amesisitiza msimamo wa serikali dhidi ya watu na mashirika yanayotoa mafunzo ya kupotosha na kusababisha mauaji ya wakenya kwa kisingizio cha dini, akitangaza kwamba kasisi huyo bandia atahukumiwa na hatapata nafasi tena nje ya Jela.
The entire 800-acre parcel of land that is part of the Shakahola ranch is hereby declared a disturbed area and an operation zone. The multi-agency security team will upscale the search and rescue mission to save as many lives as possible. pic.twitter.com/oDcgv2Q00d
— Kithure Kindiki (@KindikiKithure) April 25, 2023