Uhuru Kenyatta

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ameitaka serikali kujitenga na kujiepusha na vitendo vinavyohusu chama cha Jubilee, na badala yake kuelekeza nguvu zake katika kuimarisha maisha ya wakenya.

Akizungumza baada ya kuzuru ofisi za Chama cha Jubilee ambazo zilikuwa na purukushani siku ya leo, Kiongozi huyo mstaafu wa taifa amesuta kitendo cha serikali kuwatumia maafisa wa polisi kuwahangaisha wananchi na badala ya kuyalinda Maisha ya wananchi.

“Sisi hatuna vita na mtu. Tunalinda chama yetu na wale ambao hawataki waende tu na wakwende kwa amani hakuna haja ya kusumbua watu.” Rais mstaafu Uhuru Kenyatta

Hapo awali maafisa wa polisi walifunga njia zinazoelekea katika ofisi za chama hicho, ili kuwazuia baadhi ya wakuu wa chama hicho kufika kwenye ofisi hizo. Rais mstaafu alisema kuwa chama hicho kinafuata katiba na yeyote anayehisi kugura chama hicho ameruhusiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

 

April 26, 2023