BY ISAYA BURUGU 27TH APRIL,2023-Shughuli ya ukaguzi wa maiti zipatazo 98 zilizopatikana kule Shakahola kaunti ya Kilifi  inatarajiwa kuanza leo katika hospitali ya Malindi.Tayari mkaguzi mkuu wa maiti wa serikali amewasili Malindi kwa zoezi hilo.Ukaguzi huo unaendeshwa ili kubaini kilichopelekea vifo hivyo.

Haya yanajiri huku mhubiri bandia Paul Mackenzie ambaye watu hao walikutanana na kifo chao katika dhehebu lake la good news international akiendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Malindi uchunguzi ukiendelea.

Zaidi ya familia mia tatu zimekita kambi nje ya hospitali ya Malindi kusubiri uchunguzi  wa maiti kubaini iwapo ni jamii zao baada ya kutofanikiwa kuwapata jamaa hao wanaripotiwa Kwenda kijiunga na dhehebu Mackenzie.

.

Wakati huo huo taarifa za hivi punde zinasema kuwa mhubiri mwingine Ezekiel Odero amekamatwa kuhusiana na vifo vya watu kanisani mwake Mavueni kaunti hiyo ya Kilifi.

Haya ni kwa mjibu wa mashirikishi mkuu wa pwani Rhoda Onyancha.Kukamatwa kwa mhubiri Ezekiel wa kanis ala New life kunajiri siku moja baada yake kuhojiwa na makachero wa DCI.

 

 

 

 

April 27, 2023