BY SAIAYA BURUGU 27TH APRIL,2023-Rais William Ruto ametia Saini kuwa sheria mswada wa ugavi wa mapato wa mwaka 2023 uliopitishwa na bunge la seneti wiki jana.

Maseneta waliuzingatia na kupitisha msuada huo tarehe 20 mwezi huu bila marekebisho jinsi ulivyopitishwa na bunge la kitaiafa.Hii inazitengea kaunti shilingi bilioni 385 katika kipindi cha mwaka wakifedha 2023/24 ambacho ni kiwango cha shilingi bilioni 15 zaidi  ikilinganishwa na shilingi bilioni 370  zilizokabidhiwa kaunti zote 47 katika kipindi cha mwaka jana hadi mwaka huu.

Wakati wa kura ya wiki jana maseneta 25 walipiga kura kuitisha msuada huo bila mageuzi  na kuwashinda wenzao wa Azimio  waliotaka mageuzi kufanyiwa msuada huo na kuongeza mgao huo wa kaunti hadi shilingi bilioni 407.

Uamuzi huo hata hivyo ulikashfiwa na magavana waliowalaumu maseneta kwa kupiga kura kinume na moyo wa ugatuzi.Utiaji sahihi msuada huo kuwa sheria sasa unatoa fursa ya kuandaliwa kwa makadirio ya matumizi yakifedha kwa mwaka 2023/24.

 

 

 

 

 

 

 

April 27, 2023