shughuli ya kufukua miili katika eneo la Shakahola Kaunti ya Kilifi limesitishwa hii leo kutokana na mvua kubwa katika eneo hilo, serikali sasa ikielekeza mcho yake katika shughuli za uokozi.Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amesema kwamba serikali itafanikiwa katika vita dhidi ya magaidi wanaojificha nyuma ya dini.
Akizungumza baada ya kuzuru eneo la Shakahola katika kaunti ya Kilifi kwa mara nyingine alikoelekeza juhudi za kuimarisha operesheni ya kuwatafuta wakenya wengine walio katika msitu huo, ameeleza kwamba serikali itakabiliana na mashirika ya Imani potovu kama wanavyokabaliwa magaidi wengine na maadui wa taifa la kenya. Waziri Kindiki pia ametangaza kuwa maafisa walio katika eneo hilo wataanza kutumia ndege ili kuendeleza uchunguzi Zaidi.
Zaidi ya hayo, Waziri Kindiki ametoa onyo kwa wahubiri wanaokashifu operesheni inayoendelea, akieleza kwamba serikali haitasita katika kukabiliana na watu wanaojificha nyuma ya dini ili kuwadhulumu wakenya.