BY ISAYA BURUGU,29TH APRIL,2023-Luteni generali  Francis Omondi Ogolla  na luteni generali  Jonah Maina Mwangi wameapishwa rasmi hivi leo  kama mkuu wa majeshi  na naibu wake mtawalia katika hafla iliyoandaliwa katika ikulu ya Nairobi.Ogolla anachukua mahala pa generali  Robert Kariuki Kibochi ambaye muda wake wa kuhudumu umefikia mwisho.Generali  Ogolla hadi wakati wa kuteuliwa kwake kama mkuu wa majeshi  na rais Wiliamu Ruto  alikuwa akihudumu  kama naibu mkuu wa majeshi .

Generali Kibochi kwa mjibu wa arifa kutoka kwa wizara ya ulinzi  anaondoka baada ya kuhudumu  kwenye idara ya kijeshi kwa miaka 44.Rais Ruto katika mabadiliko hayo pia amempandisha ngazi Generali Said Farah kuwa naibu chanzela wa chuo kikuu cha ulinzi   nchini .

Brigedia   David Kipkemboi Keter alipandishwa ngazi  kuwa meja generali  na kuteuliwa  naibu mkuu wa majeshi  kitengo cha rasilimali watu na mipango.Rais pia amempandisha ngazi brigedia Stephen James Mutuku  kuwa meja generali  na kumteua kama mfanyikazi wa hadhi ya juu atakaye toa maagizo  kwenye jeshi katika chuo anua cha kitaifa cha ulinzi.

Wakati huo huo rais Wiliam Ruto amemtaka mkuu mpya wa majeshi Luteni generali  Francis Omondi Ogolla   kulihudumia taifa katika wadhifa huo wake mpya kwa taadhima ya hali ya juu.Rais akisema kuwa ana Imani kuwa Ogolla atatekeleza wajibu wake kama inavyohitajika.Amemtaka kuhakikisha kuwa maadili mema na kitaluma aliyoyapata kwenye jeshi yanaendelea jinsi yalivyo chini ya utawala wake..

April 29, 2023