Askofu wa jimbo katoliki la Ngong John Oballa Owaa amewarai vijana katika jimbo hili kujifunza zaidi kuhusu imani ya kikristu ili kuepuka na kukabiliana na mafunzo ya kupotosha kutoka kwa watu wanaojiita wahubiri na walimu wa dini.

Katika homilia yake kwenye misa ya vijana jimboni iliyoandaliwa katika kathedrali ya Mt. Yosefu Ngong mapema leo, Askofu Oballa amerejelea kisa cha mauaji yanayoshuhudiwa katika eneo la Shakahola kaunti ya Kilifi, akieleza kwamba kutoifahamu imani ni mojawapo ya vichocheo vya visa vya aina hii humu nchini.

 

April 29, 2023