Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki hivi leo amerejea Shakahola kaunti ya Kilifi kushuhudia shughuli ya uchunguzi wa miili iliyopatikana katika eneo hilo inayohusishwa na dhehebu la mhubiri Bandia Paul Mackenzie.

Hadi kufikia sasa miili 110 imefukuliwa kutoka shamba hilo.

Kindiki ameeleza kuwa serikali itaweka kila kitu wazi baada ya uchunguzi huo ikiwemo miili ambayo itapatikana bila baadhi ya viuongo akidai kuwa serikali haifichi chochote.

Uchunguzi wa miili hiyo unaendeshwa na  kikosi cha watalamu kinchongozwa na mwanapathologia mkuu wa serikali Dkt. Johansen Oduor katika makafani ya hospitali ya Malindi.

Haya yanajiri huku Mackenzie akitarajiwa kurejeshwa mahakamani hiyo kesho kukabiliana na mashataka ya mauaji baada ya siku 14 za kuwa kizuizini.Polisi walikuwa wameomba siku 30 za kuendelea kumzuilia.

May 1, 2023