Kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga amesisitiza kuwa maandamano yataendelea hio kesho Jumanne 02.Mei 2023 kama yalivyoratibiwa.
Katika ktaarifa yake alasiri ya leo, Odinga amemjibu rais akisema kwamba haki ya maandamano imekubalika kilkatiba na kwamba kila mkenya ana uhuru wa kuandaa maandamano ili kuwasilisha malalamishi yake kwa idara mbalimbali za umma. Aidha amesuta semi za viongozi mbalimbali serikalini kwa semi za kuhusisha maandamano ya upinzani na vurugu, akieleza kwamba vurugu zinazoshuhudiwa husababishwa na muingilio wa polisi katika shughuli hizi.
On our planned protest rallies, we confirm that they are on tomorrow, beginning 6 am on 2nd May 2023. #MaandamanoTuesday pic.twitter.com/MRpXXS9dAy
— Raila Odinga (@RailaOdinga) May 1, 2023
Kuhusiana na suala la vifo katika eneo la Shakahola, Odinga amemwelekezea kidole cha lawama rais William Ruto, akisema kuwa anafaa kulaumiwa kama tu wahubiri waliohusika katika utoaji wa mafunzo ya itikadi kali kama yaliyoshuhudiwa eneo la shakahola. Kiongozi huyo amesuta hatua ya rais kuanzisha jopo la uchunguzi, akieleza kwamba rais hana uwezo wowote kisheria wa kuunda jopo la aina hii.
Awali katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya Labour Day, Katibu wa chama cha wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli aliwaomba wafanyakazi kususia maandamano hayo ya upinzani na badala yake kujihusisha na ujenzi wa taifa la kenya.
As Kenyan workers, we extend our sincere appreciation to the President of the Republic of Kenya H.E Dr. William Samoei Ruto for honoring our invitation to be the Chief Guest during this 58th Labour Day celebrations at Uhuru Gardens.
Specifically, we thank His Excellency,… pic.twitter.com/T9IT4ChEq0
— Francis Atwoli NOM (DZA), CBS, EBS, MBS. (@AtwoliDza) May 1, 2023