BY ISAYA BURUGU 2ND MAY 20234-Wafuasi wa kanisa la Mhubiri  Ezekiel Odero la  New Life Prayer Centre and Church,kwa sasa wanafanya maombi nje ya mahakama ya Shanzu katika kaunti ya Mombasa.Hii ni kufuatia hali ambapo mhubiri huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo  kufahamu iwapo  atachiliwa kwa dhamana  au kuendelea kuzuiliwa kama vile upande wa mashataka ulivyokuwa umeuliza.

Mhubiri huyo alikamatwa Alahamisi iliyopita katika uchunguzi  unaohusiana na ulaghai,ulanguzi wa fedha,mauaji, kufanikisha kujitoa uhai ,uhalifu dhidi ya binadamu kati yam engine.Wafuasi wake sasa wanadai watakita kambi nje ya majengo ya mahakama  kwa nyimbo za sifa na kumwombea mhubiri huyo  aliyekamatawa kwa madai wanayosema yana nia ya kumharibia jina.

mahakama mwendo wa saa nane inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu iwapo Ezekiel ataemdelea kuzuiliwa au atachiliwa kwa dhamana.Haya yanajiri huku mawakili wa Ezekiel wakiwasilisha ombiu mahakamani  kutaka kuzuia mahakama kumzuilia Zaidi  kwa siku 30 ili kuruhusu uchunguzi unaohusiana na mauaji yam situ wa Shakahola.Wakili wake  Cliff Ombeta na  Danstan Omari, Shadrack Wambui na  Jared Magolo,wamewasilisha  ombi jipya  wakitaka mahakama kuzuiliwa kutoa uamuzi wake wakisema wanahitaji muda kusikiizwa.

Mawakili hao wakitoa wito kwa wafuasi wa mhubiri huyo ambao waliwahi leta mgonjwa wao na akafa kwenye kanisa la mtuhimishi huyo kuandikisha taarifa na polisi.

 

 

 

May 2, 2023