Wakenya 409 wamesafirishwa kutoka nchini Sudan kufikia sasa huku serikali ikiendelea na mipango ya kuwarejesha nyumbani wakenya waliosalia nchini humo.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya kigeni Alfred Mutua ni kwamba Kenya inachangia pakubwa katika juhudi za kurejesha amani nchini humo ambapo rais William Ruto aliongoza mkutano uliohudhuriwa na washirika wa umoja wa mataifa kuhusu jinsi ya kupeleka usaidizi nchini Sudan.

Zaidi ya watu 500 wameaga nchini humo tangu kuanza kwa vita hivyo huku maelfu wakilazimika kuyakimbia makaazi yao.

May 2, 2023