BY ISAYA BURUGU 03,MAY 2023-Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasili humu nchini  kufuatilia hali ya kibinadamu na kuisalama nchini Sudan kufuatia wiki za makabiliano.Bw Guterres amepokelewa na Waziri wa mambo ya nje wa Alfred Mutua katika uwanja wa ndege, wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.Katika ziara yake ya siku mbili,

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa atafanya mazungumzo na Rais William Ruto na kukutana na wakuu wote wa mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi.Makundi ya kijeshi yanayopigana nchini Sudan yamekubaliana kusitisha mapigano kwa muda wa siku saba kuanzia hiyo kesho  Alhamisi.

 Wakati huo huo Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida yuko humu nchini kwa ziara rasmi ya siku moja.Tayari amelakiwa na mwenyeji wake rais Wiliam Ruto katika Ikulu ya Nairobi.Viongozi hao wawili wanatarajiwa kutoa taarifa ya Pamoja kuhusu maswala mbali mbali yanayohusu nchi hizi mbili.Pia watafafanua Zaidi kuhusu Nyanja za ushirikiano zikiwemo uwekezaji,na ubadilishanaji wa teknologia.

 

May 3, 2023