Rais William Ruto ameratibiwa kuondoka nchini jioni ya leo kwa ziara rasmi barani ulaya. Kwa mujibu wa taarifa iiyochapishwa na Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed, rais ataanzia ziara yake nchini Uingereza, ambapo atajumuika na viongozi wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani kuhudhuria hafla ya kutawazwa kwa mfalme Charles III hapo kesho Jumamosi 06. Mei 2023.
Baadaye rais ataelekea katika taifa la Uholanzi siku ya Jumapili kwa mazungumzo na mfalme wa uholanzi William Alexander, kabla ya kukamilisha ziara yake kwa kuzuru taifa la Israel kwa siku mbili baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Waziri mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu.
Baadhi ya mambo ambayo raisa anatarjiwa kuzungumzia katika ziara zake ni Pamoja na uwezekano wa mataifa haya kushirikiana na Kenya kwa misingi ya kibiashara, ukulima, ulinzi Pamoja na maswala ya teknolojia.
Press Release: President Ruto’s official and State visit to Europe and Israel. pic.twitter.com/GkB8FUfBHm
— Hussein Mohamed, MBS. (@HusseinMohamedg) May 5, 2023