Zoezi la kufukua miili katika msitu wa shakahola imerejelewa hii leo baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa miili 110 iliyofukuliwa awali.

Maafisa wa upelelezi wa mauaji wanaendesha zoezi hilo ambalo lilisitishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha huku uchunguzi dhidi ya mhubiri wa kanisa la good news international Paul Mackenzie ukiendelea.

Mchungaji huyo wa Malindi, mkewe Rhoda Mumbua Maweu na washtakiwa wenzake 16 wataendelea kuzuiliwa na polisi hadi Mei 10 wakati mahakama itakapotoa uamuzi kuhusu ombi la serikali la kutaka kumshikilia kwa siku 90.

Washukiwa hao wamezuiliwa katika vituo vya polisi vya Malindi, Marereni na Watamu.

May 6, 2023