Kiongozi wa taifa Rais William Ruto amefanya mazungumzo na rais wa Israel Isaac Herzog nchini Isarel ambapo wawili hao wameafikiana kushirikiana hasa katika ukuzaji wa chakula.
Rais Ruto vilevile ameelezea hamu yake ya kushirikiana na taifa hilo kwenye sekta za afya, uchumi wa baharini pamoja na usalama ikizingatiwa kuwa Kenya inasaidia katika mazungumzo ya kurejesha amani katika mataifa mbalimbali.
Kenya and Israel have a uniquely strong, deep and warm relationship. We are broadening this friendship — with a special focus on agriculture — to efficiently produce more to feed our people and export the surplus. pic.twitter.com/I6kRdnziM8
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) May 9, 2023
Kiongozi wa taifa pia aliandaa kikao cha Pamoja na Waziri mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu, ambapo wawili hao wamekubaliana kukoleza mahusiano na kuimarisha biashara kati ya mataifa haya mawili.
The Kenya-Israel ties have evolved into a complex and transformational partnership. Yet, trade volumes between the two countries remain acutely low. pic.twitter.com/aeUVjn41fe
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) May 9, 2023