Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya mtoto wa kiume ,wanaharakati wa kutetea haki za watoto katika kaunti hii ya Narok wameelezea wasiwasi wao kuwa maslahi ya mtotowa kiume katika jamii yanazidi kupuuzwa kwa kiwango kikubwa.

Wamedai kwamba hali hiyo imepelekea wengi wa watoto hao wa kiume kujiingiza katika mambo ya kihalifu, utumizi wa mihadarati, kuranda mitaani miongoni mwa tabia zingine potovu.

Micheal Okiro ambaye ni mmoja wa wanaharakati hao amesema  kwamba mtoto wa kiume ameendelea kutelekezwa katika jamii huku mtoto wa kike akipewa kipau mbele.

Kauli ya Okiri imeungwa mkono na kaimu naibu kamishna eneo la Narok ya kati Abdishakurr Ali.

 

May 16, 2023